Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kupitia maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi imetekeleza miradi ya kimkakati yenye dhamira ya kukabili changamoto ya mfumko wa bei za vyakula baada ya kukamilika kwa ujenzi wa ghala kubwa la kuhifadhia chakula katika bandari ya wete mkoa wa Kaskazini pemba.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkao wa Kaskazini Pemba Mhe.Salama Mborouk Khatib,wakati akizungum na vijana wa Matembezi ya UVCCM ya kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ujenzi wa Taifa wa mradi wa nyumba ya kitega uchumi cha UVCCM Mkoa huo.
Mhe.Salama ,amesema ghala hilo limejengwa na kampuni ya Yassin provision store lenye uwezo wa kubeba tani 8,000 za vyakula na litasaidia kupunguza bei za vyakula kwa upande
wa kisiwani Pemba ambapo vyakula vya aina zote vinatarajiwa kuingizwa kutoka nchi jirani kama vile Kenya, Rwanda,Burundi na nchi nyengine za jirani ambapo amesema bei ya mchele
itapungua sana hususan kwa bei ya jumlaa kwa wafanya biashara wakubwa kisiwani pemba.
Amesema miaka 60 ya mapinduzi ya Zanzibar kwenye mkoa wake wa kaskazini Pemba jumla ya miradi 5 mikubwa imetekelezwa kwa ufanisi mkubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
chini ya Rais dk Hussein Ali Mwinyi ambapo skuli za Ghorofa saba na mbili zimekamilika na tano zipo katika hatua ya mwisho ya kukamilika .
Akizungumzia mradi wa maji safi na salama tayari umekamilika sambamba na ujenzi wa miundombinu ya barabara za ndani.
Katika maelezo yake Mhe.Salama alisema Serikali imetoa fursa za uwezeshaji wa makundi mbalimbali ya Vijana ili wajiajiri na kujiongezea kipato.
Pamoja na hao alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejenga masoko mawili makubwa katika eneo la kivumbi kai na Tumbe wilaya ya micheweni ambapo kila soko limegharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.5.
Nae Mkuu wa Matembezi hayo Mhe.Machano Ali Machano ,amesema miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar inaakiwa kuenziwa kwa vitendo kwa kuanzisha miradi ya maendeleo itakayowanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum kupiia kundi la Vijana Mkoa wa Katavi Mhe.Lucy... amepongeza jitihada za vijana kwa upande wa kaskazini pemba kwa kuanzisha miradi ambayo imewezesha kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Ndugu Hashir Ali Said,alisema mradi huo wa jengo lenye ghorofa tatu utagharimu kiasi cha shilingi milioni 470 unaojengwa katika eneo la Wilaya ya Wete.
Mradi huo ndio uliohiimisha maembezi hayo kwa upande wa Pemba na yataendelea Tarehe Januari 1,mwaka 2024 katika Mkoa wa Kusini Unguja.
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
05-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
05-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
05-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
05-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
05-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
05-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
05-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
05-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
05-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
05-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
05-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
05-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
05-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
05-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
05-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
05-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
05-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
05-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
05-03-2026
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
05-03-2026