Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dkt.Mohamed Said Dimwa, amewataka Viongozi, Watendaji na Wanachama kuepuka makundi yasiyofaa yanayoweza kuharibu umoja na mshikamano ndani ya Chama hicho
Kauli hiyo ameitoa wakati akiwahutubia Wanachama na Viongozi katika hafla ya ufungaji wa madarasa ya mafunzo ya Itikadi iliyofanyika katika Ofisi ya Tawi la CCM Miwaleni Jimbo la Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja kichama.
Alisema huu ni wakati wa wanachama na viongozi kushikamana zaidi katika kujiimarisha kisera,kisiasa na kiitikadi kwa nia ya kuendeleza utamaduni wa kuwa na wanachama wazalendo wenye kulinda maslahi ya Chama kwa vitendo.
Katika maelezo yake Dkt.Dimwa,alisema uimara wa CCM unatokana na uwepo wa wanachama waliojengewa uwezo kupitia madarasa mbalimbali ya itikadi na uzalendo na kwamba utamaduni huo unatakiwa kuendelezwa kwa kila jimbo ili kupata wanachama wapya walioiva kisiasa na kimaadili.
Alisema mkakati huo unatekelezwa kwa kufuata matakwa ya ibara ya 246 (e) inayoelekeza kufanyika kwa mafunzo ya Makada na Viongozi wa Chama kwa nia ya kuendeleza na kukuza elimu ya itikadi na uzalendo kwa wanachama wote.
“Chama chetu kimejengwa na mifumo imara ya kisiasa na kiungozi toka enzi za TANU na ASP wazee wetu waliona mbali na kutuwekea mifumo mizuri ya kuwapa mafunzo watu wanaohitaji kujiunga na CCM kabla ya kuwapatia uanachama na hiyo ndio tofauti ya CCM na Vyama vingine vya kisiasa”,alieza Dkt.Dimwa.
Dkt.Dimwa,alitoa wito kwa Maji na Wilaya za Chama Cha Mapinduzi zinazotoa mafunzo ya itikadi kuhakikisha wanafundisha na masomo ya ujasiriamali na uchumi wa buluu ili vijana waongeze ujuzi na ubunifu wa kutumia fursa zilizowazunguka kujiajiri wenyewe.
Aliwapongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi kwa kazi kubwa wanazofanya kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Bi.Mwaka Mrisho amesema Mkoa huo wamejipanga vizuri kuhakikisha wanatekeleza kwa ufanisi ibara ya tano ya Katiba ya CCM kwa kuhakikisha Chama kinashinda na kuchukua majimbo yote ya uchaguzi mwaka 2025.
Akizungumza Mwakilishi wa Jimbo la Makunduchi Mhe.Haroun Ali Suleiman,alisema lengo la kuanzisha madarasa ya itikadi ni kuongeza wanachama wapya ambao ndio mtaji wa kisiasa wa kukipatia ushindi wa ngazi zote Chama Cha Mapinduzi.
Mhe.Haroun,aliwasihi wanachama na viongozi wa jimbo hilo kuweka kando tofauti zao zilizotokana na harakati za uchaguzi uliopita na badala yake washirikiane na kujipanga kikamilifu katika kutekeleza shughuli za kijamii na kisisa kwa ujumla.
Kupitia Dkt.Dimwa,aliwakabidhi kadi za uanachama wa CCM wanachama wapya 440 waliomaliza mafunzo ya Itikadi katika Madarasa saba ya Jimbo la Makunduchi.
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
05-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
05-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
05-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
05-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
05-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
05-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
05-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
05-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
05-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
05-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
05-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
05-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
05-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
05-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
05-11-2025
ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
05-11-2025
πππ π¬ππ¦ππ¦ππ§πππ πͺπππ’π πππ ππ¨πππππππͺπ ππͺπ ππ¨πππ‘πππ§ππ π¨πͺπππ’, π¨πππππ‘ππ’ π‘π π¨πππππππ¨, π¬ππππ ππ π πππ¨π‘ππ - πππ. πππ©π¨
05-11-2025
KAENI KIMYA KAMA HAMJUI NCHI ILIKOTOKA - WASIRA
05-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefungua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya maji na uchakataji pamba cha MOLI Oil Mills Co. Ltd kilichopo Bariadi Mkoani Simiyu tarehe 16 Juni, 2025.
05-11-2025