Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amesema Serikali ya Mapinduzi haitosita kujenga miradi ya maendeleo nchini.
Mhe. Hemed ameyasema hayo alipofanya Ziara Katika Jimbo la Pangawe na Jimbo la Fuoni Wilaya ya Dimani kichama ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi katika Majimbo yote ya Uchaguzi ya Zanzibar.
Amesema Serikali ya awamu ya Nane inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeshafikia asilimia kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020- 2025 ndani ya Miaka miwili. Hivyo, ni wajibu wa Viongozi wa ngazi zote wa Chama Cha Mapinduzi kueleza mazuri yanayofanywa na Serikali yao.
Amesema ni wajibu wa kila mwananchi kuunga Mkono juhudi zinazochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ili mema mengi yaweze kutekelezwa kwa wakati.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Tanzania inapiga hatua kubwa ya maendeleo kutokana na dhamira njema ya Viongozi wake wenye chachu ya mabadiliko kwa wananchi wao.
Katika Ziara hiyo Mhe. Hemed ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Pangawe Bondeni na kueleza kukemea tabia ya baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wanaopanga safu za Uongozi wa Uchaguzi wa Dola wa mwaka 2025 na kusema kuwa CCM haitamvumilia mtu yeyote atakayejaribu kufanya kitendo hicho.
Ameeleza kuwa kufanya hivyo ni kukiuka taratibu na Kanuni za Chama na kuwavunja moyo viongozi waliopewa dhamana ya Uongozi na Chama Cha Mapinduzi. Ameendelea kukemea tabia hiyo na kuonya kwa kila atakayekiuka kanuni na taratibu za Chama taratibu za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwani kipindi hiki inapaswa kitumike katika kuimarisha Chama.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Pangawe Ndugu Dadi Juma Dadi na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Jimbo la Fuoni Ndugu Muharami Mwinyi Kombo wameeleza kuwa wanaendelea na ujenzi wa Majengo ya Kisasa ya Chama ikiwemo Matawi ili kuwawekea mazingira mazuri wanachama na viongozi wa CCM katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Magharibi B ambaye pia ni Diwani wa Wadi ya Fuoni Kipungani Khamis Hassan Haji amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kuelekeza miradi mingi ya Maendeleo katika Manispaa ya Magharibi B hasa ujenzi wa Soko la Mwanakwerekwe na Soko la Jumbi.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025