SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema utalii ni sekta kuu ya uchumi na
maendeleo unaoingiza pekee 30% ya pato la uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza na ujumbe wa watu saba kutoka kampuni ya ujenzi wa reli na uwekezaji ya China, Ikulu Zanzibar, waliofika kumtembelea, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi aliwakaribisha wawekezaji hao kuangalia fursa mbalimbali za maendeleo zilizomo nchini.
Dk. Mwinyi aliwaeleza wageni hao sekta tatu muhimu za uchumi wa Zanzibar ikiwemo Utalii, Uvuvi na Kumbi za mikutano, hivyo aliwataka kuangalia namna ya kuwekeza kwenye maeneo hayo ili kutoa ushirikinao kwaajili ya maendeleo ya Zanzibar na wazanzibari kwa ujumla.
Akiizungumzia sekta ya Utalii, Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza wawekezaji hao kwamba Zanzibar ni kisiwa cha utalii chenye vivutio vingi vya Fukwe za bahari na Hifadhi ya kimataifa ya Mji Mkongwe ambacho awali kilipokea watalii zaidi kutokaItalia na wawekezaji wengi walitumia fursa hiyo kuwekeza na baadae watu wa Ulaya Mashariki waliendelea kuingia Zanzibar, hivyo aliikaribisha Kampuni ya Ujenzi wa Reli na Uwekezaji kutoka China, kuangalia fursa ya Mji Mkongwe wenye majengo ya historia kwa kufanya uwekezaji wa hoteli za kisasa ili kuwavutia Wachina wengi kuingia Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.
Aidha, aliwaeleza pia kuangalia namna ya kuwekeza kwenye kumbi za mikutano ya kimataifa kwani Zanzibar ina maeneo mengi ya mapumziko kwa watalii na uwekezaji sambamba na kuwakaribisha kwenye uwekezaji wa visiwa vidogo ambavyo ni vivutio vizuri kwa watalii ili kutoa fursa kwa mataifa mbalimbali duniani kuja kuitembelea Zanzibar.
Dk. Mwinyi pia aliizungumzia sekta ya uvuvi na kuwaeleza wageni hao kwamba uvuvi ni sekta kiongiozi inayosadifu dhana nzima ya Uchumi wa Buluu kutona na maumbile ya visiwa vya Unguja na Pemba kuzungurukwa na bahari ya Hindi.
Hivyo aliwaeleza kuangalia zaidi uwekezaji wa uvuvi wa kina kirefu cha maji kwani Zanzibar ina rasilimali ya samaki wengi watakaosafirishwa hadi mataifa mengine duniani.
Pia, aliwaeleza kuangalia namna ya kufanya kilimo cha samaki hai ambacho mazingira ya Zanzibar yanatuhusu ustawi wa kilimo hicho. Sambamba na kuangalia uwekezaji kwenye sekta ya miundombinu ikiwemo ujenzi wa viwanja vya ndege vya kisasa, bandari na barabara zenye viwango vya hali ya juu kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Meneja mwendeshaji wa kampuni hiyo ya Ujenzi wa Reli na Uwekezaji ya China ambae pia ni mkuu wa msafara, Hao Ping Dong alimueleza Dk. Mwinyi, kampuni yao ina miradi mingi ya mandeleo na tayari imewekeza maeneo mengi duniani.
Alieleza sekta ya ujenzi ni sekta kuu inayojishulisha zaidi kwenye kamapuni yao pia wamejikita kwenye ujenzi wa viwanja vya ndege, hoteli na majengo makubwa.
Bw. Ping alieleza kufurahishwa kwakwe na uwepo wao Zanzibar yeye na wenziwe na kutoa Shukrani zake kwa Rais Dk. Mwinyi kwa kuwapokea Ikulu, Zanzibar. Hata hivyo alimuahidi Dk. Mwinyi kujenga ushirikiano mzuri baina ya Kampuni yake na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025