ASIYETII SHERIA, KATIBA NA KUWA TAYARI KUUA KWA MASLAHI BINAFSI HUO NI UGAIDI’
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira, amesema utawala bora ni kutii Katiba na Sheria za nchi, hivyo mtu yeyote asiyetii na anataka kufanikisha mambo yake binafsi kwa kuua watu huo ni gaidi.
Wasira ameyasema hayo leo Juni 22,2025 alipokuwa akizungumza katika kikao cha ndani na viongozi na wanachama wa Chama hicho Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza , ambapo amesisitiza utawala bora kwa kutii katiba na sheria za nchi badala ya kuvunja sheria kwa kisingizio cha uhuru wa demokrasia.
Wakati akieleza hayo Wasira alionesha kukishangaa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)ambacho kimekuwa na kauli mbiu yake ya 'No Reform No Election' yenye lengo la kuvuruga uchaguzi mkuu mwaka huu na kuhoji kama hawataki kupiga kura kwanini walijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.
“Asiyetii Katiba na sheria maana yake anataka nchi isitawalike, watu wapigane wenyewe kwa wenyewe, halafu wewe eti haki yako unaitaka katika mazingira ya mauaji bila kujali matokea yake, hilo haliwezekani".
Wasira alifafanua kwamba kwa akili ya kawaida unaweza kujiuliza Katiba ipo inasema kila baada ya miaka mitano unafanyika Uchaguzi Mkuu halafu anatokea mtu anasema hakuna uchaguzi.
“Anasema hivyo kwa kutumia Katiba ipi? Katiba inaeleza wazi huwezi kughairisha uchaguzi alafu wewe unasema lazima usiwepo,kutaka kuzuia uchaguzi ni kinyume na Katiba na ni kutaka kuanzisha fujo…
“Je huo ndio utawala bora? Katiba inasema kila baada ya miaka mitano tunafanya uchaguzi wewe unasema hautafanyika…utawala bora ni kutii katiba na sheria na sio kutaka kukamilisha mambo binafsi kwa kukiuka sheria za nchi.”
Wasira alisema sababu inayoweza kufanya uchaguzi usifanyike ni vita na katika nchi yetu hakuna vita,hivyo hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi na kuwahakikishia wananchi kuwa uchaguzi mkuu uko pale pale na tayari uchaguzi ulishaanza kwa wananchi kujiandikisha katika daftari la kupiga kura.
Pia alisema kaulimbiu ya ‘No Reform No Election' inaenda kufa muda si mrefu kwasababu tayari imezidiwa nguvu na Oktoba Tunatiki, na ushahidi wa hilo Watanzania wako tayari kwenda kupiga kura kwani wamejiandikisha.
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
27-11-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
27-11-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
27-11-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
27-11-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
27-11-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
27-11-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
27-11-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
27-11-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
27-11-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
27-11-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
27-11-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
27-11-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
27-11-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
27-11-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
27-11-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
27-11-2025
TAARIFA KWA UMMA
27-11-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
27-11-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
27-11-2025
MONGELLA AONGOZA MAZISHI YA KADA WA CCM JIJINI MWANZA
27-11-2025