RAIS WA ZANZIBAR MHE.DK.HUSSEIN MWINYI AHUTUBIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANI ZANZIBAR 23-7-2023.
Dk. Mwinyi aliyasema hayo ukumbi wa Golden Tulip, Uwanja wa ndege Zanzibar, kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Mwani duniani.
Alisema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha kampuni ya Mwani ya Serikali (ZASCO) ili kuleta matumaini ya kumkomboa mkulima wa mwani, kuongeza bei bora kwa wakulima wa zao hilo.
Alisema, kilimo cha mwani ni utekelezaji wa mipango ya serikali katika kuleta mageuzi kwenye sekta ya mwani nchini, kupitia uchumi wa buluu, juhudi zaidi zimeongezeka na kueleza kuwa Serikali imevutiwa na jinsi ya wakulima wa zao hilo na wananchi kwa ujumla wanavyoendelea kuitikia wito wa kauli mbiu ya Serikali na kupata mwamko zaidi katika kuzichangamkia fursa za maendeleo na ajira zinazotokana na kilimo na usarifu wa zao la mwani.
“Nakuhakikishieni Serikali yenu ipo pamoja nanyi ili kuhakikisha zao la Mwani linaendelea kuwa mkombozi wa kuleta ustawi kwa wakulima na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini kama tulivyodhamiria” aliahidi Dk. Mwinyi.
Dk. Mwinyi alieleza, mafanikio makubwa yamepatikana kutokana na kilimo cha mwani kupitia fedha za Mfuko wa Ahuweni ya UVIKO 19, Serikali imewasaidia wakulima wa mwani 5,000 kwa Unguja na Pemba kwa kuwapatia boti maalumu zenye uwezo wa kufika kina kirefu cha maji na kuhimili athari za mabadiliko ya tabianchi na ugonjwa wa ice-ice.
Alisema, licha ya mafanikio hayo ya utekelezaji wa Sera na mikakati ya Wizara ya Uchumi wa bluu na mikakati ya uzalishaji wa mazao ya baharini ukiwemo mwani, Serikali imewekeza fedha nyingi kuwasaidia wakulima na wajasiriamali wa Sekta ya Mwani.
Pia, aliwashukuru wakulima wa mwana na wananchi kwa kuifanya Zanzibar kuwa mzalishaji namba moja wa barani Afrika licha ya changamoto za UVIKO – 19, mabadiliko ya tabia nchi, ugonjwa wa ice-ice, athari za kuporomoka kwa bei ya mwani duniani, bado Zanzibar ina mchango mkubwa wa uzalishaji mwani, kwa kushindana na wazalishaji wakubwa duniani kama China, Philippines, Indonesia na wengine.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Kongano la Mwani, Zanzibar (ZaSCI) Dk. Flower Msuya aliomba ushirikiano kutoka serikalini na taasisi zake ili kuzimaliza changamoto zinazozikabili zao la mwani nchini.
Alieleza, changamoto tabianchi na bei ndogo ya zao hilo zimelisababisha kuanzishwa kwa Kongano la Mwani miaka nane iliyopita, ili kuleta ubunifu na usarifu wa mwani Zanzibar.
Dk. Flower alieleza Zanzibar kwa mara ya kwanza ilitambua bidhaa zinazotokana na zao la mwani mwaka 2006 kwa kikundi cha kwanza wanawake na kinamama kutoka Kidoti, Mkoa wa Kaskazini Unguja kuwapa elimu ya kusarifu bidhaa za zao la mwani kwa matumizi mengine ya jamii.
Kwa muijibu wa takwimu za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, uzalishaji mwani umeongezeka kutoka tani 9,663 mwaka 2019/2020, na kufikia tani 12,594 mwaka 2021/2022.
Zao la mwani lina matumizi mengi kwa usatawi wa uchimi wa Zanzibar ikiwemo chakula, vipodozi, dawa, mbolea na chakula cha mifugo.
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
22-03-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
22-03-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
22-03-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
22-03-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
22-03-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
22-03-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
22-03-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
22-03-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
22-03-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
22-03-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
22-03-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
22-03-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
22-03-2026
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
22-03-2026
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
22-03-2026
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
22-03-2026
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
22-03-2026
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
22-03-2026
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
22-03-2026
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
22-03-2026