ππππππ πππ. πππππππ ππππππ ππππππ ππ πππππππ πππππ ππππππππ ππ πππππππ ππππ ππππππ ππ πππ
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi leo tarehe 27 Januari 2025, amepokea risala ya waliowahi kuwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), iliyosomwa na Mhandisi Burton Kyaka, wakiunga mkono maazimio ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, ambao ulikutana hivi karibuni jijini Dodoma.
Maazimio hayo ni kumchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya CCM, na kumthibitisha Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwa mgombea pekee wa CCM kwenye nafasi ya Urais wa Zanzibar, katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
#CCMImara
#VitendoVinaSauti
#TunaendeleaNaMama
#KaziIendelee