RAIS DKT. SAMIA ACHANGIA SH. MILIONI 50 KUMUENZI PADRI SHIRIMA
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Seminari Uru, mkoani Kilimanjaro.
Mchango huo umetolewa ili kuweka alama ya kumbukumbu ya kumuenzi marehemu Padri Canute Mkwe Shirima AJ, aliyewahi kuwa Baba Gombera wa shule hiyo, mojawapo ya seminari maarufu nchini.
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, alitangaza mchango huo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia alipokuwa akitoa salaam za pole na rambirambi katika ibada ya mazishi ya Padri Shirima, iliyofanyika Seminari ya Uru, Alhamisi, Machi 20, 2025.
“Haya yote niliyoyasema hapa kumhusu Baba Gombera mstaafu Padri Canute Shirima, alivyokuwa mlezi mzuri akifundisha nidhamu na uwajibikaji, nilimwambia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Nilimtaarifu kuwa nakatisha ziara ili kuhudhuria mazishi haya. Mheshimiwa Rais akaniambia anatoa shilingi milioni 50 kwa Seminari ya Uru ili mtengeneze jambo lolote litakaloenzi heshima ya Padri Shirima,” alisema Balozi Nchimbi.
Akizungumzia marehemu Padri Shirima, Dkt. Nchimbi, ambaye pia aliwahi kuwa mwanafunzi wa seminari hiyo, alisema alikuwa mwalimu mahiri aliyesisitiza nidhamu na uwajibikaji kwa wanafunzi wake.
Aliongeza kuwa uongozi wa Padri Shirima ulisaidia Seminari ya Uru kupata sifa kubwa kwa kutoa wahitimu waliodhihirisha uwezo mkubwa katika nyanja mbalimbali.
“Tunawashukuru sana wazazi wa Padri Shirima kwa malezi mazuri waliyompa, ambayo nasi tuliyapata kupitia yeye. Asanteni sana Mapadri Watume wa Yesu Kristo na mapadri wote mliopo. Asante sana Baba Askofu Minde kwa heshima hii ya kuja kuongoza ibada ya kumuaga mwalimu wetu,” alisema Balozi Nchimbi.
Akiongoza ibada hiyo, Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Mhashamu Askofu Rudovick Joseph Minde ALCP/OSS, alisema marehemu Padri Shirima alikuwa zawadi ya Mungu kwa jamii aliyowatumikia.
“Kwa namna alivyoshuhudiwa hapa na umati huu uliokusanyika, mmeona na kusikia jinsi alivyolea watu wakubwa sasa, wakiwemo maaskofu, mapadri, viongozi wa juu serikalini, na hata tumepata salaam kutoka Ofisi ya Rais… Padri Canute alikuwa zawadi ya Mungu kwetu,” alisema Askofu Minde.
Padri Canute Mkwe Shirima, wa Shirika la Watume wa Yesu, ambaye alifariki akiwa katika utume nchini Afrika Kusini, alizikwa kwa heshima zote za Kanisa Katoliki katika makaburi ya Shule ya Sekondari ya Seminari Uru, Moshi, Kilimanjaro.
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
29-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
29-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
29-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
29-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
29-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
29-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
29-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
29-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
29-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
29-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
29-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
29-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
29-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
29-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
29-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
29-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
29-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
29-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
29-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
29-05-2026