BALOZI DKT. NCHIMBI AZURU KABURI LA HAYATI JOHN KOMBA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi, Jumapili, Aprili 21, 2024, amezuru kaburi la Hayati Kepteni (mst) John Damiano Komba na kutoa heshima zake kwenye kaburi hilo kwa kuweka shada la maua.
Dkt. Nchimbi ambaye ameambatana na Katibu wa NEC - Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa Ndugu. Amos Makalla, Katibu wa NEC - Oganaizesheni wa CCM Taifa Ndugu. Issa Haji Gavu pamoja na Katibu wa NEC- Uchumi na Fedha Ndugu Dk. Frank George Haule Hawassi, pia alipata wasaa wa kuwasalimia na kuwapatia pole familia, ndugu, jamaa, marafiki na wananchi wa Kijiji cha Lituhi, alipozikwa Kepteni Komba.
Hayati Komba, ambaye alikuwa mhamasishaji mkuu wa CCM, akiwa pia amefanya kazi kubwa ya nchi, kupitia kazi za sanaa, na aliwahi kuwa Mbunge wa Majimbo ya Mbinga Magharibi na Nyasa, kwa nyakati tofauti, kwa tiketi ya CCM, alifariki dunia mwaka 2015 tarehe 28 mwezi Februari.
Akiwa hapo Lituhi, Dkt. Nchimbi, amekutana na familia na wananchi wa maeneo ya karibu waliojitokeza kuungana nae katika kuzuru kaburi la Komba na kumuombea apumzike kwa amani.
”Kwa niaba ya viongozi wenzangu na wanachama wote wa CCM, tumekuja mahali hapa kuona kaburi la aliyekuwa mkuu wa vikosi vya sanaa vya CCM na ni kwa sababu ya kuthamini na kutambua mchango mkubwa katika kushiriki na kuandaa Taifa, vita ya kuitetea Tanzania dhidi ya Uganda, kutangaza na kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Ukimwi, kuimarisha sanaa kwa mziki wa jadi na wa kisasa pamoja na mengine mengi yenye msingi imara kwa Taifa letu. CCM itaendelea kuthamini na kuhakikisha aliyoyaanzisha hayati Kepteni Komba hayapotei bure,” amesema Dkt. Nchimbi.
Naye, Dkt. George John Komba kwa niaba ya familia ya marehemu Komba, amesema;
“Tunatoa shukrani kwa CCM kuanzia kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na viongozi wote wa taifa, mkoa, wilaya , kata, matawi, mashina na wajumbe wote kwa kuedelea kukumbuka kazi ya hayati Kepteni Komba ambaye kwetu ni Baba lakini kwenu ni askari jasiri ambaye amepigana na kushiriki katika kampeni za CCM kupata ushindi wa kishindo katika awamu zote.
”Familia tunawahakikishia tutaendelea kuwa wananchama waadilifu wa CCM sababu mafanikio yetu sote ni yanatokana na CCM na alituachia urithi kwa kusema isitokee hata mmoja akahama kwenda upande tofauti na CCM nasi tunaahidi kukienzi na kuwa wanachama wa hai.”
ποΈ21 Aprili, 2024
πLituhi - Ruvuma
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
29-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
29-05-2026
π° πππππππππ πππππππ πππ ππππππππ πππππππππππ
29-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
29-05-2026
π°VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
29-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
29-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE β KIBAHA
29-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
29-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
29-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
29-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
29-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
29-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
29-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
29-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
29-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
29-05-2026
πππ¦πππ‘ππ’ πππ πππ§. π ππππ₯π’ ππππ£π’πππππͺπ ππͺπ π¦πππ‘ππͺπ πππ₯ ππ¦ π¦πππππ
29-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
29-05-2026
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
29-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
29-05-2026