CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar champongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa azma yake ya kuifungua Pemba kiuchumi
CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar kimempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa azma yake ya kuifungua kiuchumi kisiwa cha Pemba.
Kauli hiyo ameitoa Katibu wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi,Zanzibar Khamis Mbeto Khamis kwenye mkutano wa Rais Dk.Mwinyi ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Halmashauri kuu za Majimbo,wilaya na mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema serikali ya awamu ya nane inatarajia kujenga uwanja wa kisasa wa ndege wa Pemba wenye urefu wa mita 2500 katika njia ya kurukia ndege. Katibu huyo alisema mbali na hilo serikali inayoongozwa na Rais Dk.Mwinyi tayari imeshafikisha huduma za umeme kwenye vijiji 65 ambapo kati ya vijiji hivyo vijiji 22 ni kutoka kisiwa cha Pemba. Alisema bajeti ijayo ya serikali itakwenda kukamilisha vijiji vingine vilivyobakia katika kufikisha huduma za umeme."Mheshimiwa Rais katika huduma za maji safi na salama takribani shehia 470 kwa Unguja na Pemba zimefikiwa na huduma hiyo muhimu,"alisema
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kusini Pemba Matar Zahor alisema eneo la sekta ya elimu serikali inayoongozwa na Rais Dk.Mwinyi katika kipindi hiki imetengeneza madarasa 158 kwenye mkoa wake ambayopo ndani yake kuna shule tatu za ghorofa na tayari zimekwishaanza kutumika. "Lakini pia mchakato unaendelea ya kuyajenga madarasa mengine kazi imeanza shule ya Ole,Michakaini na tunatarajia kupata shule ya ghorofa kwenye eneo la kengeja na Wesha,"alisema
Alisema kwa upande wa ajira mkoa wa kusini Pemba imepata ajira mpya 981 za walimu na kwamba bado kuna ajira 500 ambazo zinatarajiwa kupatikana kupitia eneo hilo la sekta ya elimu baada ya kukamilika kwa mchakato wa kuajiri.
"Katika eneo la miundombinu ya barabara mkoa wetu tunaendelea vizuri tumekamilisha hivi karibuni barabara ya Kijangwani Birikau yenye urefu wa kilomita 4.2 kwa kiwango cha lami na barabara ya Kipapo Mgelema yenye urefu wa kilomita 6.4 imeanza kuwekwa lami,"alisema
KIPINDI MAALUMU
08-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐈𝐌𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐒𝐀𝐅𝐀𝐑𝐀 𝐊𝐔𝐒𝐀𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
08-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐔𝐎 𝐂𝐇𝐀 𝐀𝐅𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐋𝐎𝐋𝐄𝐍𝐈, 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
08-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐘𝐀𝐀𝐌𝐁𝐈𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐂𝐇𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐌𝐀𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐎 𝐁𝐀𝐃𝐀𝐋𝐀 𝐘𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐍𝐃𝐀𝐌𝐀𝐍𝐎
08-06-2026
𝐌𝐀𝐏𝐎𝐊𝐄𝐙𝐈 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐓𝐈𝐁𝐔 𝐖𝐀 𝐍𝐄𝐂, 𝐈𝐓𝐈𝐊𝐀𝐃𝐈, 𝐔𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐍𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐔𝐍𝐙𝐎 𝐂𝐂𝐌, 𝐍𝐃𝐔𝐆𝐔 𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐋𝐀𝐁𝐀𝐍 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈, 𝐎𝐅𝐈𝐒𝐈 𝐙𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈
08-06-2026
𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐌𝐃𝐔𝐍𝐃𝐎!
08-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐘𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐖𝐈𝐓𝐎 𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐋𝐈𝐍𝐃𝐀 𝐌𝐀𝐀𝐃𝐈𝐋𝐈 𝐍𝐀 𝐇𝐀𝐊𝐈 𝐙𝐀 𝐖𝐀𝐓𝐎𝐓𝐎
08-06-2026
𝐊𝐄𝐍𝐀𝐍𝐈 𝐀𝐒𝐀𝐌𝐁𝐀𝐙𝐀 𝐔𝐏𝐄𝐍𝐃𝐎 𝐖𝐀 𝐀𝐆𝐀𝐏𝐄 𝐊𝐖𝐄𝐍𝐘𝐄 𝐊𝐈𝐉𝐈𝐖𝐄 𝐂𝐇𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐃𝐄𝐌𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔
08-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐀𝐍𝐙𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐊𝐀𝐆𝐔𝐀 𝐔𝐇𝐀𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐇𝐀𝐌𝐀
08-06-2026
𝐌𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐎 𝐖𝐀 𝐇𝐀𝐃𝐇𝐀𝐑𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐀𝐑𝐀𝐓𝐔 - 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐀𝐑𝐔𝐒𝐇𝐀
08-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐓𝐔𝐍𝐔𝐊𝐈𝐖𝐀 𝐒𝐇𝐀𝐇𝐀𝐃𝐀 𝐘𝐀 𝐇𝐄𝐒𝐇𝐈𝐌𝐀 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈
08-06-2026
𝐀𝐑𝐔𝐌𝐄𝐑𝐔, 𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐀𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀!
08-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐑𝐀𝐒𝐌𝐈 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈, 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐏𝐔𝐓𝐈𝐍
08-06-2026
𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎, 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐊𝐔𝐉𝐀
08-06-2026
𝐑𝐀𝐈𝐒 𝐃𝐊𝐓. 𝐒𝐀𝐌𝐈𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐌𝐎𝐒𝐂𝐎𝐖, 𝐔𝐑𝐔𝐒𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀
08-06-2026
𝐌𝐖𝐄𝐍𝐄𝐙𝐈 𝐖𝐀 𝐂𝐂𝐌 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐖𝐈𝐋𝐀𝐘𝐀 𝐘𝐀 𝐒𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐈𝐑𝐎 𝐊𝐖𝐀 𝐙𝐈𝐀𝐑𝐀 𝐘𝐀 𝐊𝐈𝐊𝐀𝐙𝐈
08-06-2026
𝐅𝐔𝐍𝐆𝐀 𝐊𝐀𝐙𝐈 𝐌𝐊𝐎𝐀 𝐖𝐀 𝐌𝐀𝐍𝐘𝐀𝐑𝐀 𝐋𝐄𝐎!!!
08-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐓𝐄𝐌𝐁𝐄𝐋𝐄𝐀 𝐒𝐇𝐈𝐍𝐀 𝐍𝐀. 𝟐 𝐊𝐀𝐓𝐀 𝐘𝐀 𝐁𝐎𝐍𝐆𝐀
08-06-2026
𝐁𝐀𝐁𝐀𝐓𝐈 𝐌𝐉𝐈𝐍𝐈 𝐋𝐄𝐎 𝐓𝐔𝐍𝐀𝐈𝐅𝐔𝐍𝐈𝐊𝐀!!!
08-06-2026
𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐊𝐔𝐓𝐀𝐍𝐀 𝐍𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐇𝐀𝐍𝐀𝐍𝐆, 𝐀𝐒𝐈𝐊𝐈𝐋𝐈𝐙𝐀 𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐀𝐓𝐔𝐀 𝐊𝐄𝐑𝐎 𝐙𝐀𝐎
08-06-2026