Serikali ya Awamu ya Nane (8) itaendelea kuboresha miundombimnu ya upatikanaji wa huduma mbali mbali ikiwemo huduma za Afya nchini ikiwa ni azma ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ya kutoa huduma bora za Afya kwa kila mwananchi bila ya malipo na ubaguzi wa aina yoyote.
Akifungua Hospitali ya Wilaya ya Kati iliyopo Mwera Pongwe , Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla amesema kupitia ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050, Sera na Mikakati mbali mbali Serikali imeweza kujenga hospitali kumi (10) za Wilaya kwa Unguja na Pemba ambazo zina vifaa tiba pamoja na magari ya kubebea wagonjwa pindi dharura itakapotokea.
Mhe. Hemed amesema miradi hii ya maendeleao inayofanywa na Serikali inaakisi malengo ya Mapinduzi ambayo ndio fikra na mawazo ya waasisi wa Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 hivyo Serikali itaendelea kuimarisha huduma bora kwa jamii kwa kuhakikisha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, TEHAMA,wafamasia, wauguzi pamoja na madaktari wakutosha katika hospitali na vituo vya Afya nchini.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameuagiza Uongozi wa Wizara ya Afya kuhakikisha wanaisimamia vyema hosptiali hio na hospitali nyengine ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali kwa kuwapatia wananchi huduma bora bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Amesema Wiza ya Afya ina wajibu wa kuhakikisha hospitali hizi zinatunzwa na kufanyiwa ukarabati wa majengo na vitendea kazi mara kwa mara ili kuviwezesha kuwa endelevu katika utoaji wa huduma na kuwataka wafanyakazi waliopangiwa katika hospital ya Mwera Pongwe
Mhe. Hemed amezitaka kampuni ya Lancet na Saifee amabazo zimepewa mkataba wa kutoa huduma hospitalini hapo kuhakikisha huduma zote zinapatikana kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu kama makubaliano yanavyoelekeza.
Sambamba na hayo amewataka wahudumu na madaktari kuendelea kutumia lugha nzuri na kufuata maadili yao ya kazi wakati wanapowahudumia wagonjwa wanaofika kupatiwa huduma hospitalini hapo pamoja na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa madaktari na wahudumu sambamba na kuilinda miundombinu iliyomo hospitalini ili iweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu.
Nae Waziri wa Afya Mhe Nassor Ahmed Mazurui amesema hudu za Afya zimeimarika zaidi Zanzibar ndani ya miaka mitatu (3) ya Uongozi wa Rais Dk Mwinyi kwa kujengwa mahospitali ya Wilaya, Mkoa na zile za Rufaa pamoja na kufanyiwa maboresho makubwa baadhi ya vituo vya Afya.
Amesema kuwa hospitali na vituo vya Afya vilivyojengwa vimekidhi viwango na ubora, pamoja na kuwepo vifaa tiba vya kutosha kulingana na uhitaji sambamba na utolewaji wa huduma za matibabu kwa wananchi wote bila ya ubaguzi na kufikia zile fikra na mawazo ya waasisi wa mapinduzi akiwemo rais wa kwanza wa Zanzibar Marehemu Sheikh ABEID AMANI KARUME.
Akitoa Taarifa ya Kitaalamu kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kati ya Mwera Ponge Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Amour Suleiman amesema Jumla ya shilingi Bilioni 9.7 zimetumika katika Ujenzi wa Mradi wa Hospital hiyo ambapo kwa wakati mmoja ina uwezo wa kulaza zaidi ya wagonjwa mia moja(100) na kupatiwa matibabu hospitalini hapo.
Amesema kuwa hospitali hiyo ya Wilaya inatoa huduma mbali mbali ikiwemo Huduma ya mama na mtoto, huduma ya maabara, huduma ya magojwa ya dharura hivyo amewataka wananchi kuendelea kuitumia vizuri hospitali hiyo kwa kutoa ushirikiano kwa madaktari na watoa huduma hospitalini hapo ili kuweza kufikia malengo ya mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 ya kutoa huduma bora kwa kila mwnanchi.
MAFURIKO YA WANANCHI WA SIHA KWENYE MKUTANO MKUBWA WA HADHARA
30-05-2026
MAPOKEZI YA KATIBU MWENEZI WA CCM NDUGU KENANI L KIHONGOSI MKOANI KILIMANJARO
30-05-2026
🔰 𝐊𝐈𝐇𝐎𝐍𝐆𝐎𝐒𝐈 𝐀𝐖𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐈𝐒𝐇𝐈𝐍𝐃𝐎 𝐊𝐈𝐋𝐈𝐌𝐀𝐍𝐉𝐀𝐑𝐎
30-05-2026
CCM INAWATAKIA HERI YA SIKUKUU YA EID AL ADHA
30-05-2026
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
30-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
30-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
30-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
30-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
30-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
30-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
30-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
30-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
30-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
30-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
30-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
30-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
30-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
30-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
30-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
30-05-2026