SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEAHIDI KUWAPATIA WAKULIMA PEMBEJEO NA HUDUMA NYENDINE ZA KILIMO ILI KUWAONDOSHEA CHANGAMOTO KUELEKEA MAPINDUZI YA KIJANI KWA UCHUMI ENDELEVU.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Nane Nane kwa mwaka 2023, yanayoendelea Kizimbani, Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema, Serikali inawajibu wa kuwawezesha vijana na wanawake kwenye shughuli zao za kilimo na kuitaka Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo kuandaa utaratibu mzuri wa kuweka takwimu zao kwa lengo la kuhakikisha inapotoa pembejeo ziwafikie wahusika kwa urahisi na kwa wakati muafaka.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kuzitengeneza barabara zote zilizomo kwenye viwanja vya Maonesho ya Nane Nane Kizimbani, kwa kiwango cha lami ili kuyaongezea hadhi Maonesho ya mwakani.
Alisema, Serikali inawajibu wa kuhakikisha ardhi ndogo ya kilimo ilioyopo inatumika kwa ufanisi ili izalishe na kuongeza tija.
“Umefika wakati tuwe na takwimu sahihi ya ukubwa wa ardhi ya kilimo tuliyonayo ili tuweze kuweka mipango mizuri ya kuitumia” Alilisistiza Dk. Mwinyi.
Akizungumzia hali halisi ya uzalishaji kilimo nchini, Rais Dk. Mwinyi alieleza Serikali imeweka jitihada mbalimbali kufanikisha sekta hiyo na kueleza kuwa na matokeo yenye tija. Alieleza ongezeko la uzalishaji wa mboga mboga na matunda nchini kutoka tani 64,820 mwaka 2021 hadi tani 66,304 mwaka 2022, muhogo umeongezeka kutoka tani 181,668 mwaka 2021 hadi tani 202,519 mwaka 2022.
Kwa upande wa mifugo Rais Dk. Mwinyi alisema, ongezeko la ng’ombe waliochinjwa kutoka 25,916 mwaka 2021 hadi 27,326 mwaka 2022, kuku waliochinjwa wameongezeka kutoka 751,073 mwaka 2021 hadi 1,130,591 mwaka 2022 na mayai yaliyozalishwa yameongezeka kutoka 15,723,843 mwaka 2021 hadi 21,659,078 mwaka 2022.
Alisema, hizo ni dalili nzuri za mafanikio katika sekta ya Kilimo na Ufugaji kwa Zanzibar.
Alieleza lengo la Serikali kufanya Maonesho ya Kilimo ni kuhimiza kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa mbinu bora za kilimo ikiwemo matumizi ya teknolojia ya umwagiliaji maji na zana za kisasa kwa madhumuni ya kuongeza uzalishaji kwa mazao ya chakula na biashara ili kupata tija zaidi na kuwapa faida kubwa wakulima na Taifa kwa jumla na kuongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo ili kuendeleza sekta ya kilimo pamoja na kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi
Hata hivyo, Rais Dk. Mwinyi aliwasihi vijana kutumia fursa ya Maonesho hayo kujifunza zaidi ili wahamasike na kujiajiri kwenye sekta ya kilimo kwa lengo la kuwa na uhakika wa chakula katika kupiga hatua za maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Akizungumza kwenye maonesho hayo, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Shamata Shaame Khamis alisema, wizara inajitahidi kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Serikali katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini kama ilivyoainishwa kwenye ibara ya 145 ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2020 – 2025.
Mapema akizungumza kwenye hafla hiyo, Katibu Mkuu Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Seif Shaaban Mwinyi aliwashauri vijana na wanawake kuzitumia fursa zinazopatikana kwenye Mradi wa mashamba makubwa ya pamoja (BBT) ulioanzishwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ili kujiendeleza kiuchumi na kuyafikia mapinduzi ya kilimo. Uzinduzi wa Maonesho ya Nane Nane kwa mwaka 2023 ulikwenda sambamba uzinduzi wa Mkakati wa kilimo chini ya kaulimbiu isemayo “Vijana na wanawake ni msingi imara wa mifumo endelevu ya chakula”
🔰VYAMA VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA VYAIMARISHA MSHIKAMANO, DKT. DIMWA AHITIMISHA MAFUNZO MAALUM
26-05-2026
KATIBU WA NEC, ITIKADI, UENEZI NA MAFUNZO CCM TAIFA NDUGU KENANI KIHONGOSI AMNADI MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ISIMANI EMMANUELA KAGANDA MTATIFIKOLO
26-05-2026
MUENDELEZO WA MAFUNZO YA VIONGOZI KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE – KIBAHA
26-05-2026
SIKU YA KWANZA YA MAFUNZO KATIKA SHULE YA UONGOZI YA MWALIMU JULIUS NYERERE LEADERSHIP SCHOOL.
26-05-2026
UFUNGUZI WA MAFUNZO YA VYAMA SITA RAFIKI VYA UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA
26-05-2026
MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA MJUMBE WA KAMATI KUU YA CPC, KOMREDI LIU HAIXING IKULU DAR ES SALAAM
26-05-2026
KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM
26-05-2026
CCM NA FRELIMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA KIUCHUMI
26-05-2026
UZINDUZI WA JENGO LA MAKAO MAKUU YA ULINZI WA TAIFA
26-05-2026
CCM YAIPA POLE MSUMBIJI KWA KUKUMBWA NA MAFURIKO
26-05-2026
INJINI YA CHAMA CHA MAPINDUZI IPO MASHINANI; DKT.MIGIRO
26-05-2026
DK.MIGIRO:CCM INAJENGWA KUANZIA NGAZI YA MASHINA SIO MAJUKWAANI.
26-05-2026
𝗞𝗜𝗦𝗛𝗜𝗡𝗗𝗢 𝗖𝗛𝗔 𝗗𝗞𝗧. 𝗠𝗜𝗚𝗜𝗥𝗢 𝗖𝗛𝗔𝗣𝗢𝗞𝗘𝗟𝗘𝗪𝗔 𝗞𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗔𝗡𝗚𝗪𝗘 𝗗𝗔𝗥 𝗘𝗦 𝗦𝗔𝗟𝗔𝗔𝗠
26-05-2026
NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AMWAKILISHA KATIBU MKUU WA CCM KWENYE MSIBA WA MBUNGE WA JIMBO LA PERAMIHO
26-05-2026
𝗩𝗜𝗝𝗔𝗡𝗔 𝗧𝗨𝗜𝗟𝗜𝗡𝗗𝗘 𝗔𝗠𝗔𝗡𝗜 𝗬𝗔 𝗡𝗖𝗛𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨 - 𝗠𝗪𝗘𝗡𝗘𝗭𝗜 𝗞𝗘𝗡𝗔𝗡𝗜
26-05-2026
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
26-05-2026
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
26-05-2026
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
26-05-2026
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
26-05-2026
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
26-05-2026