MJUMBE WA KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA NDG. HEMED SULEIMAN ABDULLA AMEPONGEZA HATUA YA VIONGOZI WA JIMBO LA MWANAKWEREKWE KWA KUWASAIDIA VIJANA KUPATA UJUZI WA KUJIKIMU KIMAISHA
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Hemed Suleiman Abdulla amepongeza hatua ya Viongozi wa Jimbo la Mwanakwerekwe kujenga kituo cha wajasiriamali ili kuwasaidia vijana kuweza kupata ujuzi na kujikimu kimaisha. Mhe. Hemed ameyasema hayo wakati alipotembelea kituo cha wajasiriamali Jimbo la Mwanakwerekwe ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai wa Chama katika Majimbo yote ya Uchaguzi ya Zanzibar. Amesema kuwepo kwa kituo hicho kunaunga mkono dhamira ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwawekea mazingira mazuri wajasiriamali.
Ameeleza kuwa kituo hicho kinasaidia kuwapatia ujuzi vijana wa Jimbo hilo na majimbo mengine na hatimae kuzalisha ajira nyingi zitakazowanufaisha vijana wa Zanzibar. Akitoa taarifa ya Kituo cha Ujasiriamali Jimbo la Mwanakwerekwe Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu. Said Saleh Said ameeleza kuwa kituo hicho kimeanza rasmi mwaka 2022 kikiwa na lengo la kuwapatia elimu ya Ujasiriamali Vijana ili waweze kujiajiri pamoja na kujikimu kimaisha na kuondokana na mawazo potevu ya kujihusisha na Vikundi viovu.
Amesema tokea kuanzishwa kwake kituo hicho kimezalisha vijana wenye taaluma na uweledi mkubwa kwa kuzalisha bidhaa zilizo bora na zenye viwango pamoja na kuanzisha kitengo cha tehama kwa ajili ya kutoa elimu ya Habari na mawasiliano. Katika ziara hiyo Mjumbe huyo wa kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amezungumza na wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi na kueleza kuwa Jimbo la Mwanakwerekwe ni miongoni mwa Majimbo yaliyonufaika na miradi mingi ya kimaendeleo ambayo itawanufaisha wananchi wote bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Aidha Mhe. Hemed amewasihi wazazi na walezi kuwasimamia vijana wao ambao wameshafikia umri wa kupata Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi kuhakikisha wanpata itambulisho hivyo pamoja na kujitokeza kwa wingi wakati wa Daftari la kudumu la wapiga kura ili kukipatia ushindi Chama Cha Mapinduzi wakati wa uchaguzi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Mwanakwerekwe Ramadhan Fatawi Issa amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuelekeza miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo hilo ikiwemo Ujenzi wa Hospital ya Wilaya ya Magharibi B, Skuli za Ghorofa, barabara za ndani, Soko la kisasa na ujenzi wa Barabara za juu (FLYOVER) zinazotarajiwa kujengwa mwanzon mwa mwezi huu.
Amesema ni dhahiri Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameamua kwa dhati kuwafikishia huduma bora wananchi wake.
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025