KATIBU wa Kamati ya NEC,Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis amesema kuwa madai ya ACT-Wazalendo ya kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) yapuuzwe na hayana mashiko kwani Serikali hiyo imeundwa kwa nguvu ya kura ya maoni ya Wananchi wote kupitia mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.
Hayo ameyasema wakati akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali kwa Waandishi wa Habari hapo Ofisi kwake Kisiwandui Zanzibar.
Alisema Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) haikuundwa kwa matakwa,hisani na ridhaa ya Chama kimoja cha ACT-Wazalendo bali ipo kwa matakwa ya Wananchi waliopiga kura ya maoni ya kukubali wote kupitia kura ya maoni na kwamba hata kujitoa katika Serikali hiyo unafuatwa mfumo ule ule wa kupiga kura ya maoni.
Kupitia Mkutano huo Mbeto,alifafanua kuwa ACT-Wazalendo wana ajenda binafsi ya kuirejesha Zanzibar katika machafuko ya kisiasa ni kutokana na vitendo na kauli zao hizo za vitisho dhidi ya Serikali iliyopo madarani.
Mbeto,alisema kama dhamira ya kujitoa katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa itatimia litakuwa sio jambo jipya kwani walishawahi kususia vikao vya Baraza la Wawakilishi na Uchaguzi wa marudio mwaka 2016 na nchi ilipiga hatua kubwa za kimaendeleo bila uwepo wao.
"Kwanza nataka ACT-Wazalendo wajue kuwa CCM na Serikali zake hazitishwi na yeyote iwe mtu,Chama cha kisiasa,kundi,taasisi ya ndani na nje ya nchi tupo imara hivyo waweke maneno ya akiba wasije kujuta juu ya maamuzi yao ya kukurupuka na mihemko ya kisiasa.
Pia Wajitoe tu Vyama vipo vingi wengine watachukua nafasi yao wasijione wao ndiyo wenye hati miliki ya Zanzibar na nchi itaendeleza kubaki salama na CCM kuendelea kuwa Chama Tawala.",alisema Mbeto.
Alitoa ufafanuzi juu ya Rais Dk.Mwinyi,kuwaita ACT-Wazalendo kuzungumza nao alisema hilo ni jambo la Kawaida Rais wa nchi kukutana na watu mbali mbali kusikiliza maoni yao kisha yeye ndo mwenye maamuzi ya kutekeleza kile anachoona kinafaa.
Alisema vikao vya Rais wa Zanzibar na ACT-Wazalendo vilikuwa vya maridhiano havina uhalali wa kisheria wa kumlazimisha Rais Dk.Mwinyi atekeleze matakwa yao na kwamba kama ipo nyaraka yoyote yenye saini za makubaliano ya pande zote mbili basi zitolewe hadharani kama wanavyotoa madai yao mengine.
Hata hivyo alieleza kuwa CCM ipo tayari kukaa mezani kusikiliza maoni,ushauri na hoja za Chama chochote cha kisiasa chenye ushauri mzuri wa kuimarisha masuala mbalimbali ya kijamii,kisiasa na kiuchumi.
Katika maelezo yake Mbeto,alisema Chama hicho cha upinzani kimefilisika kisiasa Viongozi wake hawana hoja zenye mashiko wanapodai kuwa Uchaguzi wa mwaka 2020 ulikuwa sio halali inamaana hata wao pia hawana uhalali wa kuwa katika Serikali ya SUK wanayoichafua.
Sambamba na hayo Mbeto alisema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuheshimu utawala wa Kisheria wenye kujali misingi ya haki za binadamu huku kikihubiri siasa za uwazi zenye maridhiano kwa ujenzi wa nchi
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
09-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
09-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
09-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
09-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
09-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
09-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
09-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
09-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
09-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
09-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
09-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
09-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
09-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
09-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
09-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
09-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
09-12-2025
πͺπππ¨π ππ π π¦ππππππ¨π π©ππ’π‘ππ’ππ ππππππππ ππͺππ‘π¬π ππ¨π₯π ππ π ππ’π‘π - (π ππ) πππ©π¨
09-12-2025