HADI SASA TUMEFANYA MIKUTANO 30 NA KERO 148 ZIMESHATOLEWA UFUMBUZI - MWENEZI MAKALLA
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Amos Makalla, amesema hadi kufikia sasa kupitia ziara hii ya Katibu Mkuu kutembelea mikoa sita, tayari imefanyika jumla ya mikutano 30 na vikao sita vya kamati ya siasa ambapo ahadi kubwa iliyotolewa na wananchi ni kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi wa mwaka 2025.
Mwenezi Makalla amesema wananchi wamekihakikishia Chama kupata ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pamoja na kuzoa viti vya ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu.
“ Katika ziara hiyo ya mikoa sita kazi kubwa imefanyika, tulianza ziara mkoa wa Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma kwa awamu ya kwanza ambako kote tulipopita tumepokelewa kwa kishindo. Tumefanya mikutano 30, vikao sita vya kamati ya siasa, tumeangalia uhai wa Chama na kote tulipopita wameahidi mambo mawili kuhusu uchaguzi" .
Makalla ameeleza mambo hayo ni;
" Kwanza CCM itashinda kwa kishindo uchaguzi wa serikali za mitaa, wameahidi madiwani na wabunge tutashinda kwa kishindo lakini nafasi moja ya urais fomu yake ni moja tu ya Rais Samia. Mikoa yote inasimama na Rais Samia, ahadi kubwa ni ushindi kwa CCM .”
Akizungumza kwenye mkutano wa ndani, Mwenezi Makalla amesema hadi kufikia juzi jumla ya kero 148 zimesikilizwa na kutolewa ufumbuzi huku akitumia nafasi hiyo kuwaagiza viongozi wa CCM kusikiliza kero za wananchi kisha kuzifikisha serikali kwa ufumbuzi.
“ Ofisi za CCM ni kimbilio la wananchi, wasikilizeni wananchi kisha kero zao mzipeleke katika ofisi za serikali, msiwaachie watendaji wa serikali peke yao ,” alisema Mwenezi Makalla
Vilevile, Mwenezi Makalla ameendelea kusisitiza juu ya uwepo wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri mahususi kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu.
“ WanaCCM na jumuiya zote tuhamasishe wenzetu wanufaike na mikopo hiyo kwa sababu wapinzani kwao siyo ajenda. Wapo kwenye maandamano na wanaamini vijana wao wakiwa masikini ndiyo watawatumia kwenye maandamano" .
ποΈ22 Aprili, 2024
πMbinga - Ruvuma
π©ππππ‘π π§π¨ππππ‘ππ ππ ππ‘π π¬π π‘πππ π¬ππ§π¨ - π πͺππ‘πππ πππ‘ππ‘π
14-12-2025
DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AONGOZA KIKAO MAALUMU CHA KAMATI KUU YA CCM
14-12-2025
RAIS SAMIA AKIWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI WATEULE- IKULU CHAMWINO DODOMA
14-12-2025
WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA (GENERAL)
14-12-2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ..
14-12-2025
RAIS SAMIA AKIHUTUBIA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
14-12-2025
DKT SAMIA:TUNAFANYA UCHAGUZI KWA FEDHA ZETU WENYEWE
14-12-2025
MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA MANYARA
14-12-2025
π¨ππππ£πππππ πͺπ πππ§. π¦ππ ππ π¨π ππππ§π ππ ππ‘π ππͺπ πͺππ£ππ‘πππ‘π, πͺππππ¨ππππ πππ
πππ©πππͺ ππ πͺπͺ πΏπ π©. πππππ§π€ ππ¬ππ₯π€π ππ πππ€π£ππ€π―π π¬π πΎππΌπΏπππΌ π£π πΌπΎπ
14-12-2025
πππ§. π¦ππ ππ ππ§π¨π π‘πππ‘π π¬π ππ₯πππ π¬π ππππ’π π
14-12-2025
KATIBU MKUU WA CCM, BALOZI DKT. ASHA-ROSE MIGIRO AKUTANA NA RAIS MWINYI – ZANZIBAR
14-12-2025
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM 2025-2030
14-12-2025
WASIRA:CCM HATUKATI MGOMBEA ILA TUNATEUA WACHACHE KATI YA WENGI
14-12-2025
WANACHAMA 280 WA CHADEMA WATIMKIA CCM
14-12-2025
BALOZI NCHIMBI: MAONI YOYOTE KUHUSU AMANI YA TANZANIA HAYATAPUUZWA
14-12-2025
π¦ππ₯πππππ π¬π π₯πππ¦ πππ§. π¦ππ ππ ππ ππͺπππ ππππ π π¬π π πππ‘πππππ’ ππππ π¦ππππ π¨ - ππ£π. ππ π’π¦ π ππππππ
14-12-2025
MAKALLA: BARABARA YA MPWAPWA NJIAPANDA KONGWA KUJENGWA LAMI
14-12-2025
BALOZI NCHIMBI AWASILI ARUSHA
14-12-2025
TAARIFA KWA UMMA
14-12-2025
UCHAGUZI MKUU SIO AJALI-WASIRA
14-12-2025