CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA NI UTHIBITISHO  WA KAZI KUBWA ANAZOZIFANYA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN.

alternative

Chama Cha Mapinduzi (CCM) tumeguswa na kufurahishwa na uamuzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kumtunuku shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mahafali ya 52 duru ya 5 yaliyofanyika leo Jumatano 30 Novemba, 2022 ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Uamuzi huo ni uthibitisho wa dhahiri wa kazi kubwa na nzuri zinazofanywa na serikali ya CCM, awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuleta ustawi wa maisha na maendeleo endelevu kwa Nchi yetu. 

Kati ya kazi kubwa zlizofanyika na kutumika kumtunuku shahada hiyo ya heshima ni pamoja na mageuzi ya kiuchumi, uimarishaji wa misingi ya demokrasia, utawala bora, maendeleo ya jamii, ameleta furaha na tumaini jipya miongoni mwa wananchi ambayo yote ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2020-2025 uliochagizwa na utashi wake wa kisiasa, ukomavu na umahiri alionao katika uongozi wake.

Shahada hii ya heshima ni fahari kwa  Chama Cha Mapinduzi  na watanzania wote kuwa tunaye Rais anayewajibika kwa maslahi ya wote na tunaimani ya kwamba 
itampa moyo kuwa watanzania wanaona kazi nzuri anazozifanya kwa Taifa hivyo kumpa ari na nguvu ya kuendelea kutekeleza wajibu wake.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

alternative

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50