CCM - Chama Cha Mapinduzi
Muda Wa Kazi: 24/7

Habari na Matukio Mbalimbali


TUOMBEANE KWA MAANA ZIARA HII IMEWAVURUGA KWELIKWELI WALE WOTE WANAOUTAKA URAIS 2025 NA KUIVURUGA CCM - MWENEZI MAKONDA

alternative


"Hayati Mwalimu Nyerere alisema CCM kiwe Chama Cha Sauti ya Wanyonge, kisimamie haki kwahiyo lazima nizingatie na nitahakikisha kwamba heshima yake na kazi zake nzuri alizoziifanya zinaendelea kuwa kumbukumbu katika Taifa hili"

"Tuendelee kuombeana sana kwa maana mafisadi kwenye hii nchi wapo wengi bado hawajaisha, mafisadi na wanaotaka Uongozi na wakati sifa hawana bado wapo kwahiyo wakiona nasimamia hivi utekelezaji wa Ilani lazima watataka kutuchonganisha"

"Na najua hii ziara ya kanda ya ziwa tuliyoanza nayo imewavuruga kweli na si kwa watoa taarifa tu hata wale waliopo ndani ya chama ambao wanataka kuvuruga chama na kumvuruga Rais wetu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili wao watake kuchukua nafasi ya urais , sasa nawaambie nimepewa fimbo hapa na familia ya Mwl. Nyerere nitaitumia kuwachapa kwelikweli"

alternative alternative

Maoni & Mawasiliano

Unaweza kuwasiliana na CCM, kwa kutumia anuani hapo chini kwa Maswali yoyote na Maoni.
Chama Cha Mapinduzi, Kuu Street, P.O.Box 50, Dodoma-TZ.
Barua Pepe
Muda Wa Kazi
24/7
Anuani
P.O.Box 50