JINA NA IMANI Jina la Chama litakuwa CHAMA CHAMA PINDUZI, kwa kifupi CCM. Makao Makuu ya CCM yatakuwa Dodoma na kutakuwa na Afisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar na Ofisi Ndogo ya Makao Makuu Dar es Salaam. Bendera ya CCM itakuwa na rangi ya kijani kibichi, ambayo itakuwa na alama ya Jembe (alama ya mkulima) na Nyundo (alama ya mfanyakazi) kwenye pembe ya juu upande wa mlingoti. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba: Binadamu wote ni sawa. Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake. Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.



